BAGHDAD: Watu kumi na mbili wauwawa mjini Mosul,Iraq.
23 Februari 2005Chama cha muungano cha washia nchini Iraq kimemchagua Ibrahim Aljafaari kuwa mgombea wake wa kiti cha waziri mkuu.Chama hicho kinachojulikana kama United Iraq Alliance kilishinda viti vingi katika uchaguzi wa januari 30.
Maafisa wa chama hicho wamemtaja Jafaari kuwa mgombea wao baada ya mpinzani wake ambaye anaungwa mkono na Marekani Ahmed Chalabi kujiuzulu.
Al Jafaari ni mmoja wa makamu wa rais nchini Iraq.
Jafaari mwenye umri wa miaka 53 pia ni Daktari anayeongoza chama cha Dawa Islamist Party ameishi katika hifadhi ya kisiasa nchini Iran kwa miaka mingi.Marekani imesema itafanya kazi na
yeyote atakayechaguliwa kidemokrasia kuwa waziri mkuu wa Iraq.Wakati huo huo zaidi ya watu 12 wameuwawa akiwemo mwanasiasa wa madhehebu ya shia baada ya shsmbulio la bomu la kujitoa muhanga kaskazini mwa Iraq katika mji wa Mosul.