Baghdad. Watu 25 wauwawa katika kituo cha kijeshi nchini Iraq.
11 Julai 2005Matangazo
Mshambuliaji wa kujitoa muhanga ameuwa kiasi cha watu 25 na kuwajeruhi wengine zaidi ya 12 katika kituo cha kuandisha wanajeshi wapya nchini Iraq kilichoko katika eneo la magharibi ya mji mkuu Baghdad.
Tawi la al Qaeda nchini Iraq limedai kuhusika na shambulio hilo katika taarifa iliyotolewa katika mtandao wa Internet.
Kituo cha kuandikisha wanajeshi wapya cha Muthana mjini Baghdad, karibu eneo la kati la mji huo , kimewahi kushambuliwa hapo kabla , kama sehemu ya kampeni ya wapiganaji wa chini kwa chini, dhidi ya jeshi la serikali mpya ya Iraq.