Baghdad. Wapiganaji wa chini kwa chini nchini Iraq wazidi kuleta maafa.
2 Julai 2005Matangazo
Mtu mmoja aliyejilipua kwa bomu ameuwa watu 20 nje ya kituo cha uandikishaji wa wanajeshi wapya cha wizara ya mambo ya ndani katika mji mkuu wa Iraq, Baghdad.
Wengine 20 wamejeruhiwa.
Msemaji wa wizara hiyo ya mambo ya ndani amesema wengi wa wahanga wa shambulio hilo wanaaminika kuwa ni watu waliokuwa wakijiandikisha kuwa maafisa wa polisi.
Kituo hiki cha uandikishaji kimekuwa shabaha ya wanamgambo katika siku za nyuma. Kituo kicho kiko karibu na eneo linalolindwa sana la serikali na eneo wanapofanyia kazi wanadiplomasia nchini Iraq.