BAGHDAD: Wanamgambo waendelea na mashambulio yao nchini Iraq
26 Machi 2005Matangazo
Hadi watu 16 wameuawa na wengi wengine wamejeruhiwa katika mashambulio mbali mbali yaliotokea nchini Iraq.Jemadari mmoja wa Kiiraqi ameuawa na wanae 2 wa kiume walijeruhiwa baada ya kupigwa risasi kusini-mashariki mwa mji mkuu Baghdad.Hapo kabla makomando 11 wa Kiiraqi kutoka kikosi maalum cha polisi waliuawa na watu wengi kujeruhiwa katika shambulio la bomu la gari lililofanywa na mtu aliejitolea kufa.Kwa upande mwingine mwanasiasa wa Kishia wa ngazi ya juu amesema bunge la Iraq linatazamia kukutana tena siku ya jumanne kupiga kura za kumchagua spika na makamu wawili,huku majadiliano ya kuunda serikali mpya yakiendelea kufanywa.