BAGHDAD: Wanamgambo waendelea kushambulia Iraq
24 Mei 2005
Watu 19 wameuawa na wengine wapatao kama 100 wamejeruhiwa katika wimbi jipya la mashambulio ya bomu nchini Iraq.Machafuko hayo yalitokea wakati kiasi ya wanajeshi 4,000 wa Kiiraqi na Marekani walikuwa wakiendelea kusaka maeneo yaliodhaniwa kuwa ni maficho ya wanamgambo,magharibi ya mji mkuu.Katika msako huo,hadi watu 366 wamekamatwa.Katika shambulio jingine lililofanywa na wanamgambo katika mji wa Samarra,wanajeshi 2 wa Kiiraqi waliuawa baada ya kituo cha askari jeshi kurushiwa makombora 10.Mjini Baghdad nako,Meja Jenerali Wael Rubaye,mkuu alieteuliwa hivi karibuni na serikali ya Iraq kupambana na uasi,alipigwa risasi na kuuawa alipokuwa njiani kwenda kazini.Kikundi chenye siasa kali kinacho ongozwa na mfuasi wa Al Qaeda nchini Iraq,Abu Mussab al-Zarqawi kimedai kuwa ndio kimehusika na shambulio hilo.