BAGHDAD : Wanajeshi wanne wa Uingereza wauwawa
6 Aprili 2007Matangazo
Wanajeshi wanne wa Uingereza na mkalimani wao wa Kuwait wameuwawa na bomu lililotekwa barabarani katika mji wa kusini wa Basra hapo jana.
Mwanajeshi mwengine wa sita yuko mahtuti.Wizara ya Ulinzi mjini London imethibitisha kwamba wanajeshi wawili miongoni mwa waliouwawa ni wanawake.
Wapiganaji pia wamewauwa wanajeshi 10 wa Iraq katika shambulio hapo jana kwenye kituo cha ukaguzi karibu na mji wa Mosul.
Duru zinasema takriban wapiganaji 40 walikishambulia kituo hicho wakati wa alfajiri na kuyatia moto magari pamoja na kuteka silaha za wanajeshi.