BAGHDAD: Waasi waendelea kusakwa nchini Iraq
19 Juni 2005Matangazo
Maafisa wa jeshi la Marekani wamesema zaidi ya waasi 50 wameuawa katika mashambulio mapya yenye lengo la kuwakamata wapiganaji wa kigeni nchini Iraq.Vikosi vya Marekani na Iraq vikisaidiwa na ndege za kivita,vilifanya mashambulio hayo katika bonde la mto wa Euphrates,karibu na mpaka wa Syria,ikituhumiwa kuwa katika eneo hilo kuna kambi za mafunzo za magaidi.Duru za kijeshi zimesema kiasi ya wanajeshi 1,000 wa Kimarekani na Kiiraqi wanahusika katika operesheni hii mpya.