BAGHDAD : Umwagaji damu waendelea Iraq
15 Agosti 2006Mshambuliaji wa kujitolea muhanga maisha ameuwa watu tisa katika makao makuu ya chama cha Rais wa Iraq wakati mapambano makali kati ya wafuasi wa Sheikh anayeipinga Marekani na wanajeshi wa Iraq yamesababisha kuuwawa kwa takriban watu sita leo hii.
Mshambuliaji huyo wa kujitolea muhanga maisha amejiripuwa na gari lililotegwa bomu katika eneo la kuegesha magari la makao makuu ya chama cha Rais Jalal Talabani cha Patriotic Union of Kudistan katika mji wa kaskazini wa Mosul. Watu wengine 41 wamejeruhiwa katika mripuko huo.
Katika mji wa kaskazini wa Kerbala wapiganaji wa Kiishia na majeshi ya usalama yalishambuliana kwa risasi kwa masaa kadhaa leo hii karibu na mojawapo ya makaburi matakatifu ya Iran alikozikwa Imam Hussein.