BAGHDAD: Ripota na mkalimani waachiliwa huru nchini Iraq
12 Juni 2005Matangazo
Muandishi wa habari wa Kifaraansa Florence Aubenas na mkalimani wake wa Kiiraqi Hussein Hanoun wameachiliwa huru nchini Iraq,baada ya kuzuiliwa mateka kwa muda wa miezi mitano.Wizara ya kigeni ya Ufaransa iliyotangaza habari hiyo iliongezea kuwa ripota huyo anatazamiwa kuwasili Ufaransa baadae hii leo.