BAGHDAD: Polisi wauawa mazikoni
19 Machi 2005Matangazo
Si chini ya watu saba wameuawa katika mashambulio tofauti nchini Iraq.Katika mji wa Kirkuk,kaskazini mwa nchi hadi polisi wanne waliuawa na saba wengine walijeruhiwa baada ya kuripuka kwa bomu lililofichwa kando ya bara bara.Polisi hao walikuwa njiani kwenda kumzika polisi mwenzao alieuawa siku ya Ijumaa.Vikosi vya usalama vya Iraq vinalengwa na magaidi wanaotaka kuleta vurugu katika nchi hiyo.