BAGHDAD: Polisi na wanamgambo wapambana nchini Iraq
25 Agosti 2005Matangazo
Mapambano makali yamezuka nchini Iraq,siku moja kabla ya bunge la nchi hiyo kupiga kura kuhusu mswada wa katiba mpya ya nchi hiyo.Si chini ya watu 13 wameuawa na wengine 40 wamejeruhiwa baada ya watu walioficha nyuso zao kuwashambulia polisi kwa silaha ndogo na mabomu yaliotegwa katika magari.Kwa wakati huo huo katika mji wa Najaf kusini mwa nchi,watu 5 waliuawa katika mapambano yaliozuka na wafuasi wa Moqtada al Sadr aliekuwa na siasa kali.Msemaji wa al-Sadr amesema ghasia zilianza kufuatia mashambulio yaliofanywa dhidi ya ofisi yake.Waziri mkuu Ibrahim al Jaafari katika televisheni ya taifa ameyalaani mashambulio hayo na ametoa wito wa kubakia shuari.