BAGHDAD: Operesheni ya kuwasaka waasi nchini Iraq
29 Mei 2005Matangazo
Hadi watu 3 wameuawa katika shambulio la bomu lililotokea nchini Iraq.Maafisa wa Kiiraqi wamesema mripuko huo uliotokea mapema leo asubuhi,uliulenga msafara wa magari ya vikosi vya wizara ya ndani.Polisi 1 na raia 2 waliuawa.Mripuko huo umetokea katika eneo la Madayen,kusini mwa mji mkuu Baghdad.Kwa upande mwingine hii leo,vikosi vya usalama vya Iraq vikisaidiwa na majeshi ya Marekani vimeanzisha operesheni kubwa ya usalama katika mji wa Baghdad.Kiasi ya polisi na askari jeshi 40,000 wanauzingira mji kabla ya kuanza kuwasaka waasi.Zoezi hili la kijeshi ni kubwa kabisa kupata kufanywa nchini Iraq tangu kuangushwa kwa serikali ya Saddam Hussein miaka miwili ya nyuma.