Baghdad: Mtawala wa kimarekani nchini Iraq Paul Bremer anazungumzia...
26 Novemba 2003Matangazo
mbinu mpya katika huzuma za wapiganaji wa chini kwa chini wa Iraq.Anasema hivi sasa wanamgambo wanawashambulia zaidi raia wa Iraq wanaoshirikiana na vikosi shirika,badala ya wanajeshi wa kigeni.Bwana Paul Bremer amekeumbusha mashambulio dhidi ya vituo vya polisi na kuliwa wanasiasa wa kimkoa nchini humo.Kwa upande wake jenerali John Abizaid amesema hujuma dhidi ya wanajeshi wa kimarekani zimepungua kwa kadiri nusu katika kipindi cha wiki mbili zilizopita .Na kwa mujibu wa mashahidi,mizinga kadhaa imeripuliwa jana usiku dhidi ya makao makuu ya utawala wa Marekani mjini Baghdfad.Hakuna aliyejeruhiwa.Baraza la mpito linalongozwa na Jalal Talabani limeiarifu Marekani juu ya waraka uliowasilishwa "kwa makosa" mbele ya umoja wa mataifa.Waraka huo unautaka Umoja wa mataifa upitishe azimio kuitaka Marekani iache kuikalia nchi yao."Lazma kuna makosa yaliyotokea,waraka halisi bado haujakamilika" amesema dhamana mmoja wa Marekani ambae hakutaka jina lake litajwe.Waraka halisi ulioandaliwa kwa msaada wa madhamana wa Marekani na Uengereza,ulipangwa kufikishwa mbele ya baraza la usalama kabla ya december 15 ijayo.