BAGHDAD: Mswada wa katiba ya Iraq utakuwa tayari
14 Agosti 2005Matangazo
Mswada wa katiba mpya ya Iraq unatazamiwa kuwa tayari siku ya Jumapili.Wajumbe wa jopo linalotayarisha hati hiyo wamesema kuwa baadhi ya masuala yalio muhimu bado yanahitaji kujadiliwa,lakini mswada huo utakuwa tayari.Rais wa Iraq,Jalal Talabani alipanga Agosti 15 kama tarehe ya mwisho ya kuufikisha mswada huo mbele ya bunge.Ni matumainio ya serikali ya Iraq na Washington kuwa katiba itarejesha utaratibu fulani nchini Iraq na Marekani itaweza kurejesha nyumbani sehemu kubwa ya vikosi vyake.