BAGHDAD: Mmuagiko wa damu waendelea Iraq
26 Juni 2005Matangazo
Hadi watu 28 wameuawa katika machafuko mapya yaliotokea nchini Iraq.Katika mji wa Samarra,watu 11 waliuawa na wengine 20 walijeruhiwa katika mashambulio mawili yaliolenga nyumba ya afisa mmoja wa vikosi vya polisi.Na katika mji wa kaskazini wa Mosul,polisi 4 waliuawa katika shambulio la kujitolea muhanga.Wizara ya mambo ya ndani ya Iraq imesema watu 5 walipoteza maisha yao na wengine 6 walijeruhiwa katika shambulio la kombora lililofanywa mjini Baghdad.Kwa wakati huo huo maiti za polisi 8 zimekutikana mjini Ramadi.Inasemekana kuwa polisi hao waliuawa katika shambulio la ghafla,kwenye kituo cha ukaguzi katika barabara iliyo kati ya Ramadi na mpaka wa Syria.