BAGHDAD: Miripuko 3 yatikisa mji mkuu wa Iraq
25 Oktoba 2005Matangazo
Si chini ya watu 20 wameuawa na zaidi ya dazeni wamejeruhiwa mjini Baghdad katika shambulio lililofanywa dhidi ya Palestine Hotel inayotumiwa hasa na waandishi wa habari wa kigeni.Kwa mujibu wa polisi,ukuta unaokinga hoteli hiyo ulitobolewa kwa mripuko wa lori la kuchanganyia sementi ambalo lilijazwa miripuko.Takriban wakati huo huo,miripuko miwili mingine,ilitokea karibu na hoteli hiyo hiyo,ikiaminiwa kuwa miripuko ilisababishwa na mabomu yaliyofichwa ndani ya gari.