BAGHDAD: Maziko ya mahujaji nchini Iraq
2 Septemba 2005Matangazo
Maelfu ya watu wamehudhuria maziko ya takriban mahujaji 1,000 nchini Iraq.Mahujaji hao walifariki katika mkurupuko wa ghafla uliotokea siku ya jumatano mjini Baghdad baada ya kuvuma kuwa miongoni mwa mahujaji walikuwemo washambuliaji wa kujitoa muhanga.Maiti zinaendelea kuvuliwa kutoka mto wa Tigris chini ya daraja la Aimmah,ambako msongamano ulitokea.Kwa wakati huo huo jamaa wengine wanawasaka hospitalini ndugu wanaokosekana.