Baghdad: Mauaji zaidi huko Iraq
18 Aprili 2006Matangazo
Huko Iraq si chini ya watu saba wameuwawa na 20 wengine wamejeruhiwa katika shambulio la bomu lililotokea katika mkahawa katika mji mkuu wa Baghdad. Polisi inasema bomu hilo lilifichwa chini ya kochi mlangoni mwa mkahawa huo.
Na polisi katika wilaya ya Kusini ya Dora imegundua maiti mbili za watu waliopigwa risasi vichwani. Hii imetokea siku moja baada ya maiti nyingine 12 kupatikana katika sehemu hiyo hiyo.