BAGHDAD: Mauaji yanaendelea nchini Iraq
13 Juni 2005Matangazo
Mashambulio yanayofanywa na waasi nchini Iraq yanaendelea katika pembe tofauti za nchi.
Waasi wamekishambulia Kituo cha ukaguzi kwenye barabara kuu kati ya mji wa Baghdad na Baquba hii leo.
Polisi wanne wa Iraq wameuwawa na wengine 10 wamejeruhiwa.
Watu waliokuwa ndani ya magari matatu huku wakiwa na bunduki walianza kufyatua risasi na kuwawa polisi hao na kutotokea kusini mwa mji wa Baquba.
Muda mfupi baadae bomu lililokuwa limetegwa ndani ya gari liliripuka na kuwajeruhi polisi wengine wanne.
Hii leo pia mashambulio mengine ya mabomu ya kujitoa mhanga yamefanywa katika miji ya Tikrit na Sammmara na kuwawuwa wairaqi wanane.