BAGHDAD: Mauaji nchini Iraq yanaendelea kuripotiwa
16 Juni 2005Matangazo
Kiasi cha watu 33 wameuwawa katika mashambulizi mawili tofauti ya mabomu dhidi ya wanajeshi na polisi wa Iraq.
Wanajeshi 25 wa Iraq wameuwa katika shambulizi la kujitoa muhanga lililofanywa ndani ya kantini ya wanajeshi huko kaskazini mashariki mwa mji mkuu Baghdad.
Zaidi ya wengine kumi wamejeruhiwa wengi wao wakiwa kwenye hali mbaya.
Polisi wamesema mlipuaji huyo wa kujitoa muhanga aliingia ndani ya kantini hiyo akiwa amevalia mavazi ya jeshi la Iraq na kujiripua.
Kwenye tukio jingine tofauti,watu wapatao wanane wameuwawa na wengine wengi wamejeruhiwa baada ya bomu la kutegwa ndani ya gari kuripuka kusini mwa mji wa Baghdad.Miongoni mwa waliokufa kwenye shambulio hilo ni maafisa wawili wa polisi na raia kadhaa.