BAGHDAD: Mashambulio ya wanamgambo yaendelea nchini Iraq
17 Mei 2005Matangazo
Mashambulio yanaendelea kupoteza maisha ya watu nchini Iraq.Katika mji wa Rabia si chini ya watu 5 wameuawa katika shambulio la kujitolea muhanga maisha.Mjini Baghdad pia Wairaki 2 waliuawa baada ya msafara wa magari kufyetuliwa risasi,na wengine 2 walipoteza maisha yao baada ya shule kurushiwa kombora.Vile vile katika kipindi cha saa 48,kumegunduliwa maiti za wanaume 50 katika sehemu mbali mbali za nchi.Msemaji wa serikali ya Iraq amesema,mauaji hayo yanataka kuchochea vita vya kidini,lakini serikali haitoruhusu jambo hilo.