BAGHDAD: Mashambulio ya wanamgambo yaendelea Iraq
22 Mei 2005Matangazo
Nchini Iraq afisa mwengine wa ngazi ya juu serikalini ameuawa baada ya kupigwa risasi.Mkurugenzi mkuu katika wizara ya biashara,Ali Mussa Salman na dreva wake waliuawa walipokuwa njiani kwenda kazini.Miezi hii ya nyuma,zaidi ya maafisa 12 wa ngazi ya juu wameuawa katika mashambulio ya wanamgambo.Siku ya jumamosi,waziri wa mambo ya ndani wa Iraq Bayane Baker Soulagh alitangaza mpango mpya wa usalama kwa lengo la kupambana na machafuko yanayozidi kupamba moto nchini humo.Lakini hakutaja maelezo zaidi kuhusu mpango wenyewe.Tangu kuundwa kwa serikali mpya mwishoni mwa mwezi wa April,zaidi ya watu 500 wameuawa katika mashambulio mbali mbali.