BAGHDAD: Mashambulio ya wanamgambo yaendelea Iraq
25 Julai 2005Matangazo
Si chini ya watu 25 wameuawa na wengi wengine wamejeruhiwa katika shambulio la kujitolea muhanga lililofanywa katika mji mkuu wa Iraq,Baghdad.Kwa mujibu wa majeshi ya Marekani,gari la kubebea mizigo lilipakiwa miripuko na kuripuliwa nje ya kituo cha polisi.Shambulio hilo limefanywa wakati ambapo viongozi wa madhehebu ya Kisunni wamesema kuwa wanafikiria kususia mazungumzo kuhusu katiba mpya ya Iraq.Mwito wa kususia mazungumzo hayo ulitolewa,kupinga mauaji ya viongozi wawili wa Kisunni.Wanasiasa hao wawili waliuawa na wanamgambo siku ya jumanne.