BAGHDAD-Mashambulio manne ya mabomu ya kujitoa muhanga yameua watu 66 Iraq leo peke yake.
11 Mei 2005Leo pekee kiasi cha watu 66 wameuawa katika matukio manne ya uripuaji wa mabomu ya kujitoa muhanga nchini Iraq.
Shambulio kubwa zaidi limetokea katika mji wa Tikrit,ambapo mtu aliyejitoa muhanga alijiripua akiwa ndani ya gari katikati ya umati wa watu,wengi wakiwa wafanyakazi wa Kishia.
Katika shambulio jingine lililotokea katika mji wa Hawija kusini-magharibi mwa Kirkuk,mtu mmoja aliyejisheheni mabomu,aliingia katika kambi ya jeshi iliyokuwa inaandikisha askari wapya na kujirupua.
Halikadhalika mtu mwengine aliyekuwa ndani ya gari alijiripua nje ya kituo cha polisi kusini mwa Baghdad katika kitongoji cha Dora.
Waasi nchini Iraq wanaonekana kuongeza kasi ya kampeni yao ya mashambulizi katika wiki za hivi karibuni ikiwa ni jitahada zao za kuileta hofu nchini Iraq.