BAGHDAD: Maofisa tisa wa polisi wauwawa
8 Agosti 2006Matangazo
Maofisa takriban tisa wa polisi nchini Irak wameuwawa katika mji wa kaskazini wa Samarra baada ya mshambuliaji wa kujitoa muhanga maisha kuliingiza gari lake katika kituo cha polisi. Watu wasiopungua 10 wamejeruhiwa katika shambulio hilo.
Kwingineko nchini Irak, watu yapata 12 wameuwawa kwenye mapigano kati ya jeshi linaloongozwa na Marekani na wapiganaji.
Haya yametokea huku wanajeshi wa Marekani wakijaribu kudumisha usalama mjini Baghdad katika juhudi za kuzima machafuko ya kikabila na kuwakamata wanamgambo wa makundi yanayowatesa raia.