Baghdad. Majeshi ya Marekani na yale ya Iraq yawaokoa mateka 150.
17 Aprili 2005Matangazo
Majeshi ya Marekani nchini Iraq yamefanya msako katika mji mmoja nchini humo katika juhudi za jeshi hilo kuwaokoa mateka 150 Washia waliokuwa wamekamatwa na wapiganaji wa kundi la Wasunni. Kwa mujibu wa maafisa wa polisi mateka hao ni pamoja na wanawake na watoto.
Hapo kabla majeshi ya Iraq na yale ya Marekani yaliuzingira mji wa Madaen karibu na Baghdad. Wapiganaji hao wa kundi la Wasunni wametishia kuwauwa mateka hao, huku hali ya wasi wasi ikizidi kupanda kati ya Wasunni na Washia katika eneo hilo.
Wakati huo huo kiasi cha watu zaidi ya kumi na mbili wameuwawa katika mashambulio mbali mbali nchini Iraq, ikiwa ni pamoja na wanajeshi wawili wa jeshi la Marekani.