Baghdad. Majeshi ya Marekani na Iraq yashambulia waasi.
6 Agosti 2005Majeshi ya Iraq na Marekani yakisaidiwa na ndege za kivita za Marekani yamewashambulia waasi magharibi mwa Iraq, wakifanya shambulio la hivi karibuni kabisa katika mashambulizi kadha dhidi ya wapiganaji wa chini kwa chini katika eneo tete la bonde la mto Euphrates.
Operesheni hiyo ya kijeshi , iliyopewa jina la , shambulio la haraka, imekuja siku mbili baada ya wanajeshi 14 wa Marekani kuuwawa katika shambulio la bomu lililotegwa kando ya barabara karibu na mji wa kaskazini wa Haditha, ambao ni ngome kuu ya waaasi.
Wakati huo huo , katibu mkuu wa umoja wa mataifa Kofi Annan amependekeza kurefushwa kwa muda wa ujumbe wa umoja huo nchini Iraq kwa miezi mingine 12. Muda wa sasa wa ujumbe huo unamalizika August 12.