Baghdad. Majeshi ya Iraq na Marekani yapambana na waasi.
10 Septemba 2005Matangazo
Majeshi ya Iraq na yale ya Marekani yanafanya operesheni kubwa ili kuweza kuuchukua tena mji wa kaskazini wa Tal Afar kutoka kwa waasi.
Mji huo imekuwa kwa kiasi kikubwa chini ya udhibiti wa wapiganaji wa chini kwa chini tangu majeshi ya Marekani kuivamia Iraq mwaka 2003.
Mji huo uko katika moja kati ya njia muhimu za kuingia wapiganaji kutoka Syria .
Wakati huo huo , uwanja wa ndege wa kimataifa wa mjini Baghdad umefunguliwa tena mapema leo baada ya kufungwa kwa muda wa siku moja kutokana na mzozo wa malipo kati ya viongozi wa uwanja huo na kampuni moja ya Uingereza inayotoa huduma ya usalama uwanjani hapo.